ROME : Italia yataka kuongoza kikosi Lebanon
22 Agosti 2006Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi amesema Italia iko tayari kuongoza kikosi cha kimataifa cha kulinda amani kusini mwa Lebanon.
Prodi amewaambia waandishi wa habari kwamba ametowa pendekezo hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ambaye mwishoni mwa juma hili atatowa uamuzi wa mwisho nani wa kuongoza kikosi hicho.
Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert awali aliitaka Italia kuongoza kikosi hicho cha kimataifa.