Rome. Itali wapinga hukumu ya kifo.
7 Januari 2007Matangazo
Uwanja wa mduara wa kale uliopo mjini Rome umewashwa taa kama sehemu ya kampeni ya Itali duniani dhidi ya hukumu ya kifo kufuatia kunyongwa kwa rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein.
Waziri mkuu Romano Prodi amesema kuwa juhudi hizo za Itali zitahusisha mataifa 85 wanachama wa umoja wa mataifa ambao wametia saini azimio ambalo halina nguvu ya kulazimisha Desemba mwaka jana dhidi ya hukumu hiyo ya kifo.
Kunyongwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa Iraq kumezusha wimbi la miito dhidi ya adhabu ya kifo nchini Itali na kusababisha mgomo wa kutokula kutoka kwa kiongozi wa chama mwenye msimamo mkali Marco Pannella.