ROME: Israel yasema haikulenga kituo cha Umoja wa Mataifa
27 Julai 2006Matangazo
Serikali nyingi kote duniani zimeshtushwa na kuhamakishwa na vifo vya walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa ambao hawakuwa na silaha.Maafisa hao wanne waliuawa baada ya kushambuliwa na ndege za kijeshi za Israel.Wajumbe wa Umoja wa Mataifa wameshangazwa na kutiwa wasi wasi na ukweli kwamba Israel yaonekanka kuwa ilidharau miito ya mara kwa mara kuitaka isite kukishambulia kituo hicho.Waziri wa kigeni wa Israel,Tzipi Livni amesema,kituo hicho kilipigwa kwa makosa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan hapo awali alisema,shambulio hilo laonekana kana kwamba lilidhamiria kukilenga kituo cha Umoja wa Mataifa.Maafisa wa Israel wameomba msamaha kwa shambulio hilo na wamesema wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.