1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Hakuna maafikiano kusitisha mapigano

27 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG3k

Mkutano wa kimataifa umemalizika mjini Rome bila ya makubaliano kupatikana juu ya njia ya kukomesha mapigano ya majuma mawili kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.Lakini wana diplomasia wa ngazi ya juu kutoka Ulaya,nchi za Kiarabu na Marekani walikubali kuwa kikosi cha kimataifa,chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa kinahitaji kupelekwa kusini mwa Lebanon.Waziri wa mambo ya kigeni wa Italia,Massimo Dálema amewaambia maripota kuwa wanadiplomasia hao wataendelea kutafuta njia ya kusitisha mapigano.Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema,Washington yataka kuona mapigano yakimalizika,lakini hali ya zamani ya wasi wasi na ukosefu wa utulivu wa kisiasa nchini Lebanon isirejee.Israel wala Hezbollah au wasaidizi wake Syria na Iran hawakualikwa kuhudhuria mkutano wa Rome.