Rome. Feri na meli zagongana na kusababisha vifo.
16 Januari 2007Kiasi watu wanne wameuwawa na wengine zaidi ya 90 wamejeruhiwa nchini Italia , kufuatia kugongana katika ya feri lililokuwa na abiria na meli katika pwani ya kisiwa cha Sicily.
Watu wote waliouwawa walikuwa wafanyakazi wa feri hiyo iendayo mbio, ikiwa ni pamoja na nahodha wake na fundi mchundo mkuu.
Feri hiyo iliyokuwa imebeba abiria 150 ilikuwa karibu kukatwa vipande viwili kutokana na mgongano huo na meli iliyokuwa imebeba makontena karibu na mlango wa kuingia katika bandari ya Messina. Televisheni ya taifa ya Italia RAI imeripoti kuwa meli hiyo ya mizigo ilipita katikati ya njia iliyopita feri hiyo katika eneo ambalo hupita meli nyingi.