1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Bush asikitishwa na kifo cha ajenti wa Kitaliana

8 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPS

Rais George W.Bush wa Marekani ameeleza masikitiko yake kuhusu kifo cha ajenti wa Kitaliana kilichotokea nchini Iraq.Bush alitamka hayo alipokutana na waziri mkuu wa Italia,Silvio Berlusconi kwa chakula cha jioni mjini Rome,mkesha wa maziko ya Baba Yohana Paulo wa Pili.Ajenti wa Kitaliana,Nicola Calipari,aliuawa tarehe 4 mwezi Machi nchini Iraq,baada ya vikosi vya Kimarekani kuifyetulia risasi gari yake.Ajenti huyo alikuwa akimsindikiza mwandishi wa habari wa Kitaliana Giuliana Sgrena,alie kuwa mateka na ndio kwanza aliachiliwa huru.Tukio hilo liliishtusha Italia na kuzusha hisia za hamaki dhidi ya Marekani.Tume ya Wamarekani na Wataliana inayofanya uchunguzi wa tukio hilo bado haijamaliza uchunguzi wake.