ROME: Bunge llimeidhinisha kupeleka vikosi Lebanon
27 Septemba 2006Matangazo
Bunge la Italia kwa wingi mkubwa limeidhinisha mswada unaopendekeza kupeleka hadi wanajeshi 2,500 nchini Lebanon kama sehemu ya vikosi vya kimataifa kulinda amani nchini humo.Zaidi ya wabunge 500 wameunga mkono na 20 waliupinga mswada unaohitaji sasa kupata idhini ya Senate kabla ya kuweza kufanya kazi.Italia inashika nafasi ya mbele katika mchango wa vikosi vya kimataifa na inatazamiwa kuipokea Ufaransa mwezi ujao kuviongoza vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon.