ROME : Berlusconi kuunda serikali mpya
23 Aprili 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia anayepigwa vita Silvio Berlusconi amekubali kuunda serikali mpya kuingoza nchi hiyo kutoka kwenye mgogoro wake wa kisiasa mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka minne na hiyo kuepusha kuitishwa kwa uchaguzi wa haraka.
Rais Carlo Azeglio Ciampi wa Italia amemtaka Berlusconi hapo jana kuunda serikali hiyo mpya ikiwa ni siku mbili tu baada ya kulazimishwa kujiuzulu na wenzake katika serikali ya mseto. Berlusconi amesema amefikia makubaliano na washirika wake wa kisiasa kuunda upya serikali yake ya sera za mrengo wa kulia wa wastani na anataraji kuwasilisha baraza lake la mawaziri bungeni kupigiwa kura ya kuwa na imani mwanzoni mwa wiki ijayo.