ROME : Berlusconi kukabiliwa na kura ya imani
19 Aprili 2005Matangazo
Viongozi wa baraza la senate la bunge la Italia wamesema Silvio Berlusconi atakabiliwa na kura ya imani katika baraza hilo la juu la bunge hapo Alhamisi.
Hatua hii inakuja baada ya kushindwa kujiuzulu hapo jana kama alivyokuwa akitarajiwa ili kuunda serikali mpya.Mgogoro huo ulianza Ijumaa iliopita wakati mawaziri wanne wa chama cha sera za mrengo wa kulia wa wastani UDC katika serikali ya mseto kujiuzulu wakidai mabadiliko makubwa ya sera.Mshirika mwengine katika serikali hiyo ya mseto chama cha National Alliance kinakutana leo hii kuamuwa iwapo nacho kiwaondowe au la mawaziri wake kwenye serikali hiyo.
Serikali ya mseto ya Berlusconi imeshindwa vibaya katika uchaguzi wa mikoa wa hivi karibuni.