1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME. Berlusconi atumbukia matatani.

15 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMj

Chama cha Christian Democrats, UDC, nchini Itali kimejiondoa kutoka kwa serikali ya mseto ya waziri mkuu Silvio Berlusconi. Mawaziri wanne wamejiuzulu kutoka kwa baraza lake la mawaziri, akiwemo makamu waziri mkuu, Marco Follini. Chama hicho kimetangaza kitaendelea kuiunga mkono serikali ya Berlusconi. Hata hivyo wadadisi wanasema waziri mkuu atalazimika kujiuzulu na kutafuta amri mpya ya kuendelea kutawala. Hatua ya chama hicho inafuatia kushindwa vibaya kwa serikali katika uchaguzi wa mikoa uliofanyika juma lililopita, ambao baada yake chama cha UDC kilimhimiza Berlusconi kuunda serikali ya sera mpya za maongozi.