ROME: Berlusconi ashinikizwa kuunda serikali mpya
16 Aprili 2005Matangazo
Chama cha UDC nchini Italia kimejitoa kutoka serikali ya mseto ya waziri mkuu Silvio Berlusconi.Mawaziri 4 wamejitoa serikalini ikiwa ni pamoja na makamu waziri mkuu Marco Follini.Chama hicho lakini kimesema kitaendelea kuiunga mkono serikali,ingawa hatua iliyochukuliwa inatazamwa kuwa ni jeribio la kumshinikiza Berlusconi ajiuzulu na aunde serikali mpya yenye sera tofauti.Hii ni baada ya serikali kushindwa vibaya sana wiki iliopita katika chaguzi za mikoa.Berlusconi alichaguliwa mwaka 2001 akiongoza muungano wa vyama vinne na kutoa ahadi kuwa atafanya mageuzi na kunyanyua uchumi wa nchi uliozorota.