1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME. Berlusconi ashinda kura ya imani serikalini.

29 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIP

Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi, ameshinda kura ya imani katika serikali yake mpya. Lakini swala linaloulizwa nchini humo ni kwa muda gani zaidi atakapoendelea kuuongoza muungano uliogawanyika.

Wakati huo huo, Berlusconi ametoa onyo kali kwa Marekani na akaapa kwamba Itali haitaidhinisha ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya afisa wa usalama wa Itali, Nicola Calipari yaliyofanywa na wanajeshi wa Marekani mjini Baghdad tarehe 4 mwezi uliopita.