1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME. Berlusconi asema uhusiano ka ya Itali na Marekani hautaathirika.

5 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGQ

Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi amesema nchi yake itaendelea kuwa na wanajeshi wake nchini Irak licha ya kuuwawa kwa afisa wake wa usalama na wanajeshi wa Marekani mjini Baghdad.

Berlusconi aliliambia bunge la Itali kwamba tofauti zilizozuka kati ya Marekani na Itali kuhusiana na mauaji ya Nicola Calipari, hazitoathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Calipari aliuwawa kwa kupigwa risasi alipokikaribia kituo cha jeshi la Marekani mjini Baghdad, wakati alipokuwa amembeba mateka wa rehani Giuliana Sgrena ambaye alikuwa ameokolewa kutoka mikono ya watekaji nyara.