1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Berlusconi anyakwa vibaya katika chaguzi za mikoa

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQD

Waziri mkuu wa Uitalia Silvio Berlusconi ameshindwa vibaya katika chaguzi za mikoa.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,chama cha Berlusconi kinachoelemea bawa la kulia kimepoteza mikoa 11 kutoka jumla ya 13,kikibakiwa na mikoa ya Lombardy na Veneto tu kaskazini mwa nchi.Chama kilichofaidika ni cha kushoto ya kati kinachoongozwa na Romano Prodi.Matokeo ya mwisho ya chaguzi hizo zilizofanywa siku ya Jumapili na ya Jumatatu yanatazamiwa hii leo.