1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Berlusconi ameunda serikali mpya

23 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKB

Waziri mkuu wa Uitalia,Silvio Berlusconi ameunda serikali mpya ya mseto.Tanagazo hilo limemaliza mgogoro wa kisiasa wa wiki kadhaa nchini humo.Sasa serikali mpya ya Berlusconi katika muda usiotimiza hata mwaka mmoja,itajaribu kuchangamsha uchumi uliozorota,kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa mwezi wa Mei mwaka 2006.Katika serikali mpya,wizara za mawasiliano,afya,viwanda na utamaduni zitaongozwa na mawaziri wapya.Berlusconi alijiuzulu rasmi siku tatu za nyuma baada ya washirika wake kujitoa kwenye serikali ya muungano,iliyoshindwa vibaya sana katika chaguzi za mikoa hivi karibuni.