ROME: Berlusconi ameunda serikali mpya ya mseto
24 Aprili 2005Matangazo
Rais Silvio Berlusconi wa Uitalia ameunda serikali mpya ya mseto.Serikali mpya iliyoapishwa itakuwa madarakani kwa muda usiotimiza hata mwaka mmoja kwani uchaguzi mkuu unatazamiwa kufanywa mwezi wa Mei mwaka 2006.Katika serikali mpya, wizara za mawasiliano,afya,viwanda na utamaduni zina mawaziri wapya.Berlusconi alijiuzulu rasmi siku tatu za nyuma baada ya washirika wake kujitoa kwenye serikali ya muungano,iliyoshindwa vibaya sana hivi karibuni katika chaguzi za mikoa.