ROME: Berlusconi ajaribu kuiokoa serikali yake
18 Aprili 2005Matangazo
Serikali ya mseto nchini Italia imetoa muito kwa mawaziri walioasi kurejea katika baraza la mawaziri ili serikali isije kuvunjika.Ikiwa serikali itavunjika,basi waziri mkuu Silvio Berlusconi atalazimika kuitisha uchaguzi mapema, ikisemekana kuwa Berlusconi hatoweza kupata ushindi.Hatima ya serikali yake inayumba-yumba tangu chama cha UDC kujitoa serikalini siku ya Ijumaa,kikitaka mageuzi makubwa ya kisiasa,baada ya serikali ya muungano kushindwa vibaya sana katika chaguzi za mikoani.