ROME: Baba mtakatifu Yohana Paulo wa 2 arejea Vatikan
14 Machi 2005Matangazo
Baba mtakatifu Yohana Paulo wa pili tayari amewasili Vatikan baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Mamia ya waumini walimiminika katika barabara za kuelekea Vatikan kumkaribisha baba mtakatifu aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Gemeli mjini Rome kufuatia upasuaji aliofanyiwa koo lake.
Mapema hapo jana baba mtakatifu mwenye umri wa miaka 84 alizungumza kupitia dirishani katika Hospitali alikokuwa amelazwa na kuwatakia waumini waliokuwa nje ya Hospitali hiyo jumapili njema.