ROME: Baba mtakatifu kuhudhuria ibada ya Pasaka
7 Machi 2005Matangazo
Baba mtakatifu yohana paulo wa pili anaendelea kupata nafuu na anatarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitalini kabla ya wiki inayoelekea sikukuu ya Pasaka.
Hata hivyo kwa mujibu wa Vatikan baba mtakatifu hajaamua atachukua jukumu gani wakati wa ibada ya kuadhimisha sikukuu hiyo.
Ingawa Wasaidizi wake wanatafuta njia za kutoa matangazo ya moja kwa moja kutoka Vatican yatakayoonyesha ibada hiyo ya Pasaka.