ROME: Baba mtakatifu arejea Rome
22 Agosti 2005Matangazo
Baba mtakatifu Benedikt wa 16 amerejea mjini Rome baada ya ziara ya siku nne katika nchi yake ya uzawa Ujerumani, ambapo alishiriki katika tamasha la vijana lililofanyika katika mji wa Cologne.
Vijana laki nane, hasa wa kikatoliki kutoka nchi karibu mia mbili walishiriki katika tamasha hilo.
Baba mtakatifu amewanasihi vijana hao kuepuka uhitilafu wa kujichagulia yale wanayoyataka tu na kuyapuuza mambo mengine ya dini.
Ziara ya Papa Benedikt nchini Ujerumani ilikuwa ya kwanza katika nchi za nje tokea achaguliwe kuwa kiongozi wa wakatoliki wote duniani, mnano mwezi wa aprili.
.