ROME: Baba Mtakatifu apewa heshima za mwisho
5 Aprili 2005Matangazo
Waombolezaji wanaendelea kutiririka katika kanisa la Mtakatifu Petro kutoa heshima zao za mwisho kwa Baba Mtakatifu Yohana Paulo wa Pili.Mazishi yamepangwa kufanywa siku ya Ijumaa saa nne asubuhi.Inakadiriwa kuwa hadi viongozi 200 wa kimataifa watahudhuria maziko hayo.Miongoni mwa viongozi hao ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan na Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani.Kama ilivyo desturi ya Vatikan,Papa Yohana Paulo wa Pili atazikwa katika Kanisa la Mtakatifu Petro na sio nchini Poland alikozaliwa.Hapo awali kulikuwepo uvumi kuwa atazikwa Krakow,Poland.Misa ya wafu ya Baba Mtakatifu Johana Paulo wa Pili itasomwa na Kadinali wa Kijerumani Joseph Ratzinger.