ROME: Baba Mtakatifu ametawazwa rasmi
25 Aprili 2005Matangazo
Baba Mtakatifu Benedikt wa XVI katika misa ya kuadhimisha kutawazwa kwake kama kiongozi mpya wa Kanisa la Katoliki,ametoa muito kwa Wakristo kuwa na umoja.Siku ya jumapili,katika misa iliyosomwa kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro,Kadinali wa zamani wa Ujerumani,Joseph Ratzinger,alitawazwa rasmi kama Papa wa 265,mbele ya viongozi wa kimataifa na umati uliokadiriwa kufikia laki tatu na nusu.Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 78 aliuambia umma uliokusanyika kuwa yeye ni mtumishi mnyonge wa Mungu na ametaka aombewe kusaidiwa na Mungu katika kazi kubwa mno,iliyopindukia uwezo wa binadamu.Baadae alizunguka katika gari lililokuwa wazi na kuwapungia wahujaji waliomshangilia kwenye uwanja Mtakatifu wa Petro.