1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Baba Mtakatifu ameeleza binafsi masikitiko yake

17 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBL

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 binafsi ameeleza masikitiko yake kuhusu hasira iliyoibuka miongoni mwa Waislamu kwa sababu ya matamshi yake ya hivi karibuni kuhusu Uislamu.Wakati wa mahubiri ya kila Jumapili kwenye nyumba yake ya mapumziko Castel Gandolfo karibu na Rome,Baba Mtakatifu ameeleza kuwa dondoo alilotumia siku ya Jumanne, haliakisi maoni yake ya binafsi.Amesema,maneno yake,yakichukuliwa kwa ujumla,ni mualiko wa kufanywa majadiliano ya ukweli na uaminifu.Katika hotuba yake,siku ya Jumanne,Papa alimnukuu mfalme wa Byzantine wa karne ya 14 aliesema kuwa baadhi ya mafunzo ya Mtume Muhammad yalikuwa ovu na si ya kiutu.Matamshi hayo yalisababisha wimbi la hasira katika nchi za kiislamu na makundi mengi yalitoa wito wa kumtaka Papa binafsi aombe radhi.