1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME: Baba mtakatifu akosa kuhudhuria misa ya ijumaa kuu.

25 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTi

Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili amekosa kuhudhuria misa za mwanzo wa pasaka kwa mara ya kwanza kutoka ashike uongozi wa kanisa katoliki miaka 26 iliyopita.

Baba mtakatifu aliangalia ibada ya Ijumaa kuu iliyosomwa kwa niaba yake katika televisheni, kifungu cha kwanza cha ujumbe wa baba mtakatifu alisema kuwa yuko pamoja kiroho na kimawazo na wale wote waliokusanyika katika kanisa kuu la St Peter’s Vatikan.

Baba mtakatifu Yohana Paul wa pili anatarajiwa kuongoza baraka ya Urbi et Orbi siku ya jumapili lakini hataongoza ibada katika sikukuu ya pasaka ambayo ina umuhimu mkubwa katika kalenda ya kikristo ambapo wakiristo kote duniani wanaadhimisha kusulubiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo.