ROME : Ajali ya ndege ya Sicily sio shambulio la kigaidi
7 Agosti 2005Matangazo
Watu 13 wameuwawa na wengine watatu hawajulikani walipo baada ya ndege iliokuwa imewabeba watalii wa Kitaliana kuelekea Tunisia kuanguka baharaini nje ya mwambao wa Sicily nchini Italia.
Sababu hasa ya ajali hiyo iliotokea hapo jana haikuweza kujulikana mara moja lakini rubani wa ndege hiyo aliripoti juu ya matatizo ya engine.Wizara ya uchukuzi ya Italia imekanusha uwezekano wa ajali hiyo kusababishwa na shambulio la kigaidi.
Abiria 23 kati ya 39 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ya engine mbili aina ya jeti ATR – 72 waliokolewa baharini na mashua za uokozi.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka mji wa kusini wa Italia wa Bari kuelekea katika mji wa mapumziko ya watalii wa Tunisia wa Djerba.