ROME: Ahadi ya kutuma vikosi Lebanon itimizwe
23 Agosti 2006Ujerumani imetoa mwito wa kuwepo mshikamano katika Umoja wa Ulaya kuhusu vikosi vya kimataifa vitakavyopelekwa Lebanon kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung alipozungumza na gazeti la Kitaliana amesema,Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na mstari wa mbele katika ujumbe wa Lebanon na kuonyesha umoja kwa kutimiza ahadi ya kuunda jeshi hilo.Mawaziri wa kigeni wa nchi za Umoja wa Ulaya,siku ya Ijumaa watakuwa na mkutano wa dharura mjini Brussels. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan anatazamiwa kuhudhuria mkutano huo kabla ya kuelekea Mashariki ya Kati.Italia imesema itatimiza ahadi yake ya kuongoza vikosi hivyo na kupeleka wanajeshi wake wapatao 3,000 ikiwa Israel itaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.