ROMA.Zaidi ya wahamiaji 400 wamewasili katika kisiwa cha Lampedusa
23 Oktoba 2006Matangazo
Utawala nchini Italia umetoa taarifa ya kuwasili zaidi ya wahamiaji 400 kutoka Afrika katika kisiwa cha Lampedusa.
Bado uraia wa watu hao haujajulikana lakini inaaminika walianzia safari yao kutoka pwani ya Libya.
Wakati huo huo wahamiaji 29 wameokolewa kutoka pwani ya Uhispania katika visiwa vya Canary.
Utawala nchini humo umesema kuwa idadi ya wahamiaji katika pwani za nchi hiyo imeongeza maradufu katika kipindi cha mwaka mmoja.