1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA.Wahamiaji wasio halali wawasili katika kisiwa cha Lampedusa

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0D

Utawala nchini Italia umetoa taarifa juu ya kuwasili takriban wahamiaji 300 wasio halali kutoka Afrika ya kaskazini katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

Wahamiaji hao yaaminika wametoka katika pwani ya Libya.

Kisiwa cha Lampedusa kina sehemu maalum ya kuwahifadhi wahamiaji ambao baadae hufanyiwa uchunguzi iwapo wana sababu za kutosha za kupewa hifadhi ya kisiasa.

Wale wasio timiza mahitaji yanayotakikana hupewa amri ya kurudi makwao.

Wakati huo huo wafuasi wanaounga mkono upinzani nchini Italia wamefanya maandamano dhidi ya pendekezo la bajeti ya serikali ya nchi hiyo.

Katika hotuba yake, kiongozi wa upinzani na waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi ameikosoa sera ya matumizi ya fedha za serikali ya waziri mkuu wa sasa Romano Prodi.

Bunge la Italia linatarajiwa kupiga kura juu ya bajeti hiyo ya kwanza ya waziri mkuu Prodi tangu alipochukua mamlaka.

Bajeti hiyo inalenga kubana matumizi na kuongeza kodi kufikia kiwango cha Euro bilioni 40.