Romania yaonesha ishara ya kuingiliwa anga yake.
30 Septemba 2023Wizara ya Ulinzi ya Romania imesema rada za jeshi lake zimebaini kile kinachoweza kuwa uingiliwaji wa anga ya kimatiafa wakati wa mashambulizi ya usiku kucha ya ndege zisizo na rubani za Urusi dhidi ya miundombinu ya kiraia ya Ukraine.Baada ya kujiondoa katika mpango wa kusafirisha nafaka wa Bahari Nyeusi katikati ya Julai, Urusi ilianza kushambulia bandari na maghala ya Ukraine katika maeneo ya Mto wa Danube kutokea kwa mwanachama huyo wa ushirikiano wa kijeshi wa NATO Romania. Eneo hilo linatazwama kama mbadala mkuu wa serikali ya Kyiv wa kusafirisha bidhaa zake.Lakini pamoja na rada za Romania kugundua uwezekano huo wa ukiukwaji wa sheria za kimataifa kwa kuingiliwa kwa anga yake, lakini hakuna mabaki ya ndege hizo za Urusi katika ardhi ya taifa hilo, na kwamba juhudi za kuyatafuta zinaendelea.Maafisa wa NATO na wa Romania wamesema hakuna ushahidi unaonesha kwamba mashambulizi hayo ya Urusi yanailenga Romania, na kusema hayana maana yoyote bali yanalenga kuvuruga amani.