1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roman Herzog, rais wa zamani wa Ujerumani, afariki

10 Januari 2017

Ofisi ya rais wa Ujerumani imesema Herzog, ambaye alikuwa mwanasiasa wa kwanza kufanywa rais baada ya Ujerumani Mashariki na Magharibi kuungana tena, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 82.

https://p.dw.com/p/2VYNx
Rais wa zamani wa Ujerumani, Roman Herzog
Picha: Getty Images/A. Rentz

Kabla ya kuwa rais wa Ujerumani kuanzia mwaka 1994 hadi 1999, Herzog alihudumu kama Rais wa Mahakama ya Katiba ya Ujerumani. Mwanasiasa huyo wa chama cha Christian Democratic, CDU, alifanya kampeni bila kuchoka kuhusu mageuzi na anajulikana kwa hotuba yake ya mwaka 1997 iliyokuwa na lengo la kushinikiza mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Herzog alizaliwa mwaka 1934 kwenye mji wa Landshut katika jimbo la Bavaria na alijiunga na chama cha CDU mwaka 1970 na kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi katika kipindi cha miaka mitatu iliyofuata.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW