ROMA: Waziri wa mambo ya nje wa Italy abatilisha uamuzi wake.
17 Machi 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Italy Silvio Berlusconi anaoneka kulegeza uamuzi wake alioutangaza hapo jana wa kuanza kuvihamisha vikosi vya jeshi la nchi yake kutoka Iraq kufikia mwezi september.
Amekiuka usemi huo na badala yake amesema kuwa tarehe maalumu haijulikani na iwapo vikosi vya jeshi la Italy vitaondoka Iraq basi itakuwa kwa makubaliano na washirika wenzake, Marekani na Uingereza.