1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roma: Wawakilishi wa kile kijulikanacho kama "pande nne zinazosaka ...

11 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFsw
ufumbuzi wa mzozo wa Mashariki ya kati,Marekani,Umoja wa mataifa , Umoja wa Ulaya na Rashia walikutana kwa mazungumzo jana usiku mjini Roma-nchini Italy.Duru za Marekani zimesema hii leo."Wamezungumzia hali namna ilivyo katika uhusiano kati ya Israel na Palastina pamoja na matukio ya hivi karibuni"duru hizo zimesema.Hakuna uamuzi uliopitishwa mwishoni mwa mkutano huo wa Roma.Mkutano huo umeitishwa pembezoni mwa mkutano wa wafadhili wa maeneo ya utawala wa ndani,ulioitishwa na Italy-mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya.Marekani iliwakilishwa na naibu waziri wa nje anaeshughulikia mashariki ya kati William Burns.Mawaaziri wa mambo ya nchi za nje wa Israel na Palastina walisema hapo awali mjini Roma wanafanya juhudi za kuwakutanisha waziri mkuu Ariel Sharon na mwenzake wa Palastina Ahmed Qorei haraka iwezekanavyo. Mkutano wa wafadhili unatazamiwa kumalizika baadae hii leo mjini Roma.Wapalastina wanataraji kujipatia kitita cha Euro bilioni moja nukta mbili ili kuufufua uchumi na kugharimia huduma za jamii katika ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza.