ROMA. wapelelezi wa Uingereza wafika Italia kumuhoji mtuhumiwa wa mabomu ya julai 21
10 Agosti 2005Matangazo
Wapelelezi kutoka Uingereza waliwasili mjini Roma kushirikiana na wenzao wa Italia katika shughuli ya kumuhoji mtuhumiwa wa mashambulio ya mabomu viza ya mjini London ya julai 21.
Osman Hussein ama kwa jina jingine Hamdi Issac alihojiwa kwa masaa matatu mjini Roma siku ya jumamnne mbele ya wakili wake.
Osman alisisitiza kwamba milipuko aliyoibeba na ambayo haikulipuka ilikuwa ni ya kuleta mfadhaiko tu na wala haikuwa na uwezo wa kuuwa.
Wakili wake pia ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo amekiri kuwa anawafahamu watuhumiwa wengine wa shambulio hilo viza la julai 21.
Osman mzaliwa wa Ethiopia alisafiri hadi mjini Roma Italia baada shambulio hilo viza na kukamatwa baadae mjini humo.