1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Waliosababisha kifo cha Calipari waadhibiwe

9 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYe

Italia haijakubaliana na maelezo yaliotolewa na jeshi la Kimarekani kuhusu kifo cha ajenti wa upelelezi wa Kitalaina kilichotokea Ijumaa iliyopita karibu na Baghdad nchini Iraq.Waziri wa kigeni Gianfranco Fini ameliambia bunge la Italia kuwa Washington inapaswa kuwataja na kuwaadhibu wale waliompiga risasi Nicola Calipari.Ajenti huyo alikuwa akimsindikiza ripota wa Kitaliana alieachiwa huru na watekanyara wake,gari yao ilipofyetuliwa risasi na vikosi vya Kimarekani.Jeshi la Kimarekani limesema gari hiyo ilikuwa ikienda kwa mbio na haikusimama kwenye kituo cha ukaguzi kama ilivyoamriwa kufanya.Kamanda wa majeshi ya kimataifa nchini Iraq,Jemadari George Casey wa Marekani amewaambia maripota katika wizara ya ulinzi ya Marekani-Pentagon kuwa tume ya Wamarekani na Wataliana itafanya uchunguzi kamili kuhusu tukio hilo.Amesema uchunguzi huo unatazamiwa kumalizika katika muda wa wiki tatu hadi nne.