ROMA: Ripota Sgrena arejea Italia
5 Machi 2005Matangazo
Mwandishi habari wa Kitaliana amewasili nyumbani baada ya kuzuiliwa mateka nchini Iraq kwa zaidi ya mwezi mmoja.Guiliana Sgrena aliachiliwa huru siku ya Ijumaa,lakini alijeruhiwa begani baada ya wanajeshi wa Kimarekani kuifyetulia risasi gari iliyokuwa ikimpeleka uwanja wa ndege wa Baghdad.Mtumishi wa Idara ya Ujasusi ya Italia aliekuwa akimsindikiza aliuawa.Jeshi la Marekani limesema msafara huo wa gari ulidharau kusimama kwenye kituo cha ukaguzi licha ya kuonyeshwa ishara ya kufanya hivyo.Rais George W.Bush wa Marekani ameahidi kuwa tukio hilo litachunguzwa kikamilifu.