ROMA: Ripota ajeruhiwa baada ya kuachiliwa huru
6 Machi 2005Mwandishi habari wa Kitaliana Giuliana Sgrena aliekuwa mateka kwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Iraq amerejea Roma.Ripota huyo mwenye umri wa miaka 57 ameeleza vipi vikosi vya Kimarekani vilivyoifyetulia risasi gari yake ilipokaribia kituo cha ukaguzi cha jeshi.Bibi Sgrena alijeruhiwa begani na afisa wa usalama wa Kitaliana aliehusika na juhudi za kuachiwa huru Sgrena aliuawa.Jeshi la Kimarekani limesema vikosi vyake vilifyetua risasi baada ya gari hiyo kudharau kusimama kwenye kituo cha ukaguzi licha ya kuonyeshwa ishara ya kufanya hivyo.Lakini Sgrena aliwaambia maripota kuwa gari haikuwa na mwendo mkubwa na wala hakuona ishara zo zote zile za kuonywa.Rais Silvio Berlusconi wa Italia alimuita balozi wa Marekani na amemtaka atoe maelezo kamili kuhusu tukio hilo.Rais George W.Bush wa Marekani alieleza masikitiko yake na ameahidi kuwa utafanywa uchunguzi kwa ukamilifu.