1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Rais Abbas yumo mjini Roma

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7T

Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, yumo mjini Roma Italia kwa ziara rasmi. Wakati wa ziara yake rais Abbas atakutana na kiongozi wa kanisa katoliki, baba mtakatifu Benedict wa 16, na waziri mkuu wa Italia, Romano Prodi.

Rais Abbas yumo katika ziara ya mataifa saba kutafuta uungwaji mkono kwa serikali ya mpya ya umoja wa kitaifa ya mamlaka ya Palestina.

Katika mazungumzo yake na waziri mkuu Romano Prodi na waziri wa mashauri ya kigeni wa Italia, Massimo D´Alema, rais Abbas atajaribu kuishawishi serikali ya mjini Roma na Umoja wa Ulaya umalize mgomo wao dhidi ya serikali ya Palestina.

Misaada kwa Palestina ilisitihswa wakati chama cha Hamas kilipoingia madarakani mnamo mwezi Januari mwaka jana lakini rais Abbas anataka misaada ianze kupelekwa kwa Wapalestina kwa sababu serikali mpya ya sasa inajumulisha wanachama wa chama cha siasa za wastani cha Fatah.