Roma. Prodi amtaka Olmert kuimarisha hali ya wakaazi wa Gaza.
14 Desemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amemtaka waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert kuimarisha hali ya maisha ya wakaazi wa Gaza. Viongozi hao wawili walikutana mjini Rome jana Jumatano kujadili hatua za amani za mashariki ya kati.
Prodi pia amemtaka Olmert kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.
Hapo mapema Olmert alikuwa na mazungumzo na kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Benedict 16 ambapo amemtaka kiongozi huyo wa Wakatoliki kuwataka Wakristo kupinga dhidi ya wale wanaokataa mauaji ya halaiki dhidi ya Wayahudi ya Holokaust .