Roma: Pope Benedikt wa 16 aingojea kwa hamu ziara yake ya hapa Ujerumani
3 Septemba 2006Matangazo
Pope Benedikt wa 16 amesema anaingojea kwa hamu ziara yake ijayo katika nchi yake ya Ujerumani ambayo itakuwa pamoja na kusimama kwamuda mfupi mjini Munich na katika kijiji alikozaliwa. Ziara hiyo itafanywa baina ya Septemba 9-14 na itakuwa pamoja na siku moja ambapo Pope atakuwa pamoja na ndugu yake huko Regensburg, na kuzuru makaburi ya wazazi wake na dada yake. Katika ziara hiyo, Baba Mtakatifu atasheherekea pia misa za hadhara katika miji ya Munich, Regensburg, Alteotting na Freising. Agosti mwaka jana alikuweko hapa Ujerumani kuhudhuria Siku ya Vijana Duniani mjini Kolon.