1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Papa Benedict wa XVI ataka mapigano ya Lebanon yakome

30 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG2Q

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Benedict XIV ametoa mwito mapigano ya Lebanon yakome.

Akiuhutubia umati wa watu waliokusanyika nje ya nyumba yake ya mapumziko nje ya mji wa Roma Italia, kiongozi huyo amewataka wahusika katika vita vya Lebanon waweke silaha zao chini.

Wakati huo huo, shirika la chakula duniani, WFP, limesema limelazimika kufutilia mbali msafara wa magari sita yaliyopangwa kupeleka misaada ya chakula na madawa katika mji wa Marjayoun kusini mwa Lebanon, kufuatia hatua ya jeshi la Israel kukataa.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Roma, mratibu wa misaada ya dharura wa shirika la WFP nchini Lebanon, Amer Daoudi, amesema wamevunjwa moyo na uamuzi huo wa Israel kwani watu wengi wataendelea kuteseka.