1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Papa asalia amani ya dunia

25 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpR
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katolika duniani Papa YOHANA PAULO wa Pili ametoa mwito wa kudumishwa amani kote duniani katika wito wake wa sala za kusheherekea sikukuu ya Noeli. Katika hotuba yake iliosomwa ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter mjini Roma, Papa YOHANA PAULO alikumbusha kuwa damu nyingi imemwagika ulimwenguni na hivyo kuwaomba walimwengu kukomesha uhasama na chuki baina yao. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 83 amemuomba Mungu aibariki dunia na kuitenga na wimbi la ugaidi huku akisuma risala akiwa ameketi. Papa YOHANA PAULO amekuwa akipinga vita dhidi ya Iraq na kutoa lawama zake dhidi ya kuendelezwa machafuko katika miji mitakatifu ya Mashariki ya kati.