1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roma na Madrid:Wakimbizi wa Kiafrika wawasili Italy na Spain.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CBIX

Mtiririko mkubwa wa wakimbizi wa Kiafrika kuja Ulaya haujasita. Karibu na mwambao wa Sicily, walinzi wa mwambao wa Italy waliwaokoa wakimbizi 19 kutokea Eritrea. Shirika la habari la Ansa la Italy lilisema Waafrika hao walikuwa siku 12 njiani baharini. Wanane kati yao walikufa njiani. Pia katika visiwa vya Kanary wamekwama wakimbizi kadhaa waliofika huko na mashua. Katika masaa ya karibuni wamewasili katika visiwa hivyo vya Spain zaidi ya wahamiaji 300 haramu, wengi wao walisafiri katika boti zilizo mbovu.