ROMA: Mwandishi wa habari aachiliwa huru
20 Machi 2007Matangazo
Mwandishi wa habari raia wa Italia aliyekuwa akizuiliwa kwa majuma mawili na wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan ameachiliwa huru.
Waziri mkuu wa Italia, Romano Prodi, amethibitisha kwamba Daniele Mastrogiacomo yuko katika hali nzuri kiafya na anatibiwa katika hospitali inayosimamiwa na Italia mkoani Helmand kusini mwa Afghanistan.
Daniele alitekwa nyara mapema mwezi huu alipokuwa njiani kwenda kukutana na kamanda wa Taliban.
Wanamgambo hao walitishai kumuaa mwandishi huyo ikiwa viongozi watatu wa Taliban walio gerezani hawataachiliwa huru na serikali ya Afghanistan.