1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Marekani ibebe jukumu la kifo cha Calipari

10 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYH

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi ameitaka Marekani ibebe jukumu la mauaji ya ajenti wa upelelezi wa Kitalana.Berlusconi amewaambia wabunge mjini Roma kuwa wananchi wa Italia wana haki ya kujua kile kilichotokea.Nicola Calipari alifariki baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Kimarekani alipokuwa akimsindikiza ripota wa Kitaliana alieachiwa huru na wateka-nyara.Askari jeshi wa Kimarekani na Wataliana walionusurika wametoa maelezo kuhusu tukio hilo yanayotofautiana.