1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roma: Marehemu 498 wabarakiwa na kanisa katholiki huko Vatikani

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bp

Vatikani imefanya sherehe kubwa kabisa hadharani kuwahi kuonekana ikiwabariki watu 498 waliosumbuliwa kutokana na imani zao za kidini kabla na wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Spain katika miaka ya thalathini. Hiyo ni hatua ambayo kwamba watu hao wataweza baadae kutangazwa kuwa watakatifu. Kikundi cha maaskofu 71 wa Spain, mahujaji na wanasiasa walikusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Peter. Hatua hiyo imefanyika katika kipindi ambapo uhusiano baina ya Spain na Vatikani uko katika hali tete kufuatia kanisa katholiki kupinga hatua kadhaa zilizochukuliwa na serekali ya kisoshalisti ya Spain, ikiwa ni pamoja na kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja na kulainisha sheria za talaka. Pia serekali hiyo imelilaumu kanisa kwa kumuunga mkono mdikteta wa zamani wa kifashisti katika Spain, Francisco Franco.