1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roma: Maandamano Italy kupinga kupanuliwa kituo cha kijeshi cha Kimarekani nchini humo.

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR5

Maelfu ya watu waliandamana katika mji wa Vicenza, kaskazini ya Italy, wakipinga kupanuliwa kituo cha jeshi la Marekani katika eneo hilo. Watu wenye siasa za mrengo wa shoto waliompigia kura waziri mkuu Romano Prodi mwaka jana wanatuhumu kwamba amewadanganya kwa vile ameikubalia mipango ya Marekani ya kukipanua kituo hicho. Bwana Prodi anadai uamuzi huo ulikuwa umeshakamilishwa na mtangulizi wake, Silvio Berlusconi. Hakujatokea michafuko katika maandamano hayo. Ubalozi wa Marekani umwaonya raia wao wauepuke mji huo wa Vicenza.