ROMA: Livni ataka jeshi la kimataifa litumwe haraka Lebanon
24 Agosti 2006Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni, ameitaka jamii ya kimataifa ifanye haraka iwezevyo ipeleke kikosi cha jeshi la Umoja wa Mataifa kulinda amani kusini mwa Lebanon.
Livni ameiambia runinga ya Sky 24 nchini Itali kwamba hali ni tete kusini mwa Lebanon na jukumu liko mikononi mwa mahakama ya Umoja wa Ulaya.
Tzipi Livni alikuwa mjini Roma alikokutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Itali, Massimo D´Alema. Baadaye alitarajiwa kukutana na waziri mkuu, Romano Prodi, ambaye yuko likizoni mjini Tuscan.
Wakati huo huo, wizara ya mambo ya kigeni ya Denmark imesema waziri Livni ataitembelea Denmark mnamo Agosti 28 na 29.
Wakati wa ziara yake atazungumza na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo, Per Stig Moeller, kuhusu hali ya Lebanon na utekelezwaji wa azimio 1701 la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano nchini Lebanon.
Viongozi hao pia watajadili hali katika maeneo ya Paletina.