ROMA: FAO yaonya juu ya balaa la nzige barani Afrika
11 Oktoba 2006Matangazo
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, limezionya nchi za magharibi na kaskazini mwa Afrika kuwa katika hali ya tahadhari juu ya uwezekano wa kuzuka wimbi la nzige ambao waliyaharibu mashamba ya maeneo hayo mwaka wa 2004.
Nzige wamekuweko katika sehemu za Mauritania na wanataga mayai yatakayoangua nzige wachanga katika muda wa siku 10 zijazo. Taarifa ya shirika la FAO imezionya nchi kama Algeria, Mali, Moroko na Senegal na imezitaka zichuke hatua ya tahadhari.
Balaa la nzige la mwaka wa 2004 lililigharimu shirika la FAO dola milioni 400 kukabiliana nalo na kuwaangamiza nzige hao.