1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Chama cha National Alliance kitamuunga mkono Berlusconi.

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKX

Huko Italy Silvio Berlusconi yuko tayari kupokea agizo rasmi kutoka kwa rais Carlo Azeglio Ciampi wa Italy la kuunda serikali mpya.

Berlusconi alijiuzulu wadhfa wa uwaziri mkuu siku mbili zilizopita kufuatia kushindwa vibaya kwa serikali yake ya mseto katika uchaguzi.

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Italy na kiongozi wa chama kikuu cha pili cha upinzani Gianfranco Fini ametangaza kuiunga mkono serikali mpya ya Silvio Berlusconi.

Uamuzi huo wa chama cha National Alliance ulisubiriwa kwa hamu kubwa kwani hapo awali kilitoa tishio la kuwaondoa mawaziri wake kutoka kwenye serikali ya muungano baada ya kuzuka sintofahamu katika muundo wa serikali ya Silvio Berlusconi ambae hatimae alijiuzulu.