1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA. Berlusconi kutangaza serikali mpya ya Italy baade leo.

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKf

Waziri mkuu wa Italy aliyejiuzulu Silvio Berlusconi anatarajiwa kutangaza baraza jipya la mawaziri katika seriakali mpya ya Italy jioni leo baada ya msukosuko wa kisiasa nchini humo uliomlazimu kujiuzulu.

Berlusconi amefikia makubaliano ya kuunda mseto na vyama viwili vikuu vya kisiasa nchini Italy UDC na chama cha mrengo wa kulia cha National Alliance baada ya muundo wa mseto aliokuwa akiuongoza kushindwa vibaya katika uchaguzi uliopita mwanzoni mwa mwezi huu.